Na Judith Siaga
Licha ya Shirika la Afya Ulimwenguni kuripoti kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Corona , elimu ya chanjo ya Uviko-19 bado inahitajika kwa jamii.
Ni wazi ripoti hii ya kupungua kwa maambukizi imechangiwa na watu kuchanja chanjo ya Uviko-19 hivyo ni muhimu kwa Serikali ya Tanzania kuhimiza wananchi kuchanja kwa wingi ili kutokomeza kabisa janga hili ambalo limeleta athari kubwa za kiuchumi na kuchukua maisha ya watu.
Ni ukweli usiopingika kwasasa nchini Tanzania wananchi wamesahau kabisa kuchukua tahadhari, ukitaka Kuthibitisha hili tazama kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu hawavai barako , hawanawi mikono ukiuliza kwanini watakujibu Corona imepungua.
Nitoe pongezi kwa Wizara ya Afya chini ya Waziri Ummy Mwalimu wanafanya kazi kubwa sana ya kuhamasisha jamii kuchanja chanio ya Uviko-19 kupitia mpango wa Taifa wa chanjo.
Hivyo basi natoa wito kwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa chanjo ya Uviko-19 kwani Corona bado ipo , Wananchi tuchukue tahadhari.