BENKI YA KCB YAENDELEA KUTIMIZA NDOTO ZA WAFANYABIASHARA, YAFANIKISHA UZINDUZI WA KIWANDA CHA MAFUTA YA ALIZETI SHINYANGA


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia kutoka shinnyanga, Giritu Nhila Makula (kulia)
wakati wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha  mafuta ya kupikia aina ya  kiitwacho Gilitu Enterprises LTD wengine ni Dkt. Kulwa Meshack (Aliyevaa barakoa) na Mkuu wa kitengo cha biashara za kati na ndogondogo wa Benki ya KCB, Abdul Juma (wa kwanza kushoto) hafla imefanyika katika Viwanja vya Kiwanda hicho Mkoani Shinyanga.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario  akizungumza kabla  ya kuzindua kiwanda cha  mafuta ya kupikia aina ya alizeti  kiitwacho Gilitu Enterprises LTD , Mkoani Shinyanga .
Mkurugenzi wa kiwanda cha Gilitu Enterprises LTD Giritu Nhila Makula,  akizungumza kabla  ya kuzindua kiwanda cha  mafuta ya kupikia aina ya alizeti  kiitwacho Gilitu Enterprises LTD , Mkoani Shinyanga .

Mkurugenzi wa kiwanda cha Gilitu Enterprises LTD Giritu Nhila Makula,  akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario kabla  ya kuzindua kiwanda cha  mafuta ya kupikia aina ya alizeti  kiitwacho Gilitu Enterprises LTD , Mkoani Shinyanga  .
Mkurugenzi wa kiwanda cha Gilitu Enterprises LTD Giritu Nhila Makula,   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na viongozi mbalimbali wakiwsili katika Viwanja vya Kiwanda cha Gilitu kwaajili  ya kuzindua kiwanda cha  mafuta ya kupikia aina ya alizeti  kiitwacho Gilitu Enterprises LTD , Mkoani Shinyanga .

Viongozi mbalimbali wa Benki ya KCB, Mkurugenzi wa kiwanda cha Gilitu Enterprises LTD Giritu Nhila Makula, wakimuomba Mwenyezi Mungu kabla ya kuanza zoezi la uzinduzi wa kiwanda cha  mafuta ya kupikia aina ya alizeti  kiitwacho Gilitu Enterprises LTD , Mkoani Shinyanga , 
Mkurugenzi wa kiwanda cha Gilitu Enterprises LTD Giritu Nhila Makula,  akimtembeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na viongozi mbalimbali kuona maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho kabla ya kuanza zoezi la uzinduzi 

PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO BENKI YA KCB 

*******************************************

NA YUSUPH DIGOSSI- SAUTI ZA MTAA BLOG 

Watanzania wametakiwa kuacha kasumba ya kupenda bidhaa kutoka nje ya nchi badala yake wanunue bidhaa zinazozalishwa Tanzania ili kuinua uchumi wa nchi.

Ushauri huo umetolewa na Gilitu Nila MKula Mkazi wa Geita ambaye amethubutu kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula aina ya Alizeti kinachoitwa  Gilitu enterprises LTD huku akisisitiza kuwa siri ya mafanikio ni kujiamini na kuwa na uthubutu. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kiwanda hicho Mwanzilishi huyo amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kununua mafuta yanayozalishwa ndani nchi ya Tanzania kwasababu kuna wazalishaji wengi wanaozalisha bidhaa kwa ubora wa halivya juu ambazo unakidhi viwango vya kimataifa. 

" Watanzania wengi tumekua na tabia ya kutojimini kuwa tunaweza na kuamini kuwa masuala ya Uwekezaji Kama haya yanafanywa na watu wa nje pekee jambo ambalo sio kweli" amesema Bw. Gilitu 

Ameongeza kuwa cha msingi ni wazalishaji wa ndani kuzingatia viwango vya ubora ili kuendelea kuvutia wanunuzi wa bidhaa ili kufuta dhana ya mafuta bora yenye viwango ni yale yanayotoka nje pekee.

KWANINI KIWANDA CHA MAFUTA YA ALIZETI NA SI KINGINE? 


Gilitu amesema kuwa alifikiria kuwekeza kwenye kiwanda hicho kwakuwa mafuta hayo ni salama na hayana madhara kwa mtumiaji.

" Nirifikiria kuwekeza kwenye kiwanda cha mafuta ya aliezeti kwasababu ni bora zaidi kwa afya ya mtumiaji , hivyo tuzidi kuwahimiza Watanzania wanunue bidhaa za wazalishaji wa ndani ili kuinua uchumi wa Watanzania " amesema Bwa Gilitu .

WITO KWA SERIKALI 

Bw. Gilitu Nila MKula ameiomba Serikali kuendelea kuwahimiza Watanzania kununua mafuta yanayozalishwa na wazawa yenye ubora unaostahili ili kuwainua kiuchumi. 

MCHANGO WA KCB BANK KWENYE UZINDUZI WA KIWANDA HICHO 

Benki ya KCB imeendelea kuwa mkombozi kwa Wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa kutokana na utaratibu wao wa kuendelea kutoa mikopo yenye masharti rafiki kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuwainua kiuchumi. 



Katika kufanikisha Mtanzania huyu aliyethubutu kuingia katika Uwekezaji huu Benki hii imeunga juhudi hizi  kwa kutoa  pesa za kununulia mitambo na vifaa kwaajili ya uzalishaji na uchakataji wa mafuta ya Alizeti 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Cosmas Kimario amesema kuwa wameendelea kuunga mkono juhudi za wafanyabiashara ili kwenda sambamba na kasi ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia  ya kujenga uchumi   wa Viwanda.

VIPI KUHUSU VIWANDA VINGINE

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema mbali na kiwanda walichokizindua mkoani hapo wameendelea kuviunga mkono viwanda mbalimbali mkoani Dar es Salaam kwa kuwapa mikopo iliyo nafuu itakayowasaidia kuzalisha viwanda vingi na kuongeza uzalishaji nchini;

“Mbali na kiwanda hicho, vipo viwanda vingine ambavyo tumekuwa tukivisaidia ambavyo vipo Dar es salaam ambapo tunazungumza na wateja ili kuwapa mikopo ambayo ni nafuu itakayoweza kuwasaidia kutengezeza viwanda, kuzalisha ndani na kuwaondolea serikali mzigo wa kutumia fedha za kigeni kuagiza vitu kutoka nje” amesisitiza

WITO WA KBC BANK KWA WAFANYABIASHARA 

Mkuu wa kitengo cha Biashara ndogo na Kati Abdul Juma amesema wito wao kwa wafanyabiashara ni kwamba Benki hiyo ipo tayari kufanya kazi na wafanyabiashara wa madaraja yote hadi ngazi za chini.

Amesema kuwa Benki hiyo ina wataalamu wa kibenki ambao wamebobea katika ushaurivwa masuala wa kifedha hivyo Wafanyabiashara wametakiwa kufika KCB ili waweze kupatiwa ushauri wa masuala ya kifedha ikiwemo namna ya kutunza fedha, kufanya biashara kwa faida pamoja na kutafuta masoko ya uhakika.

"Milango ipo wazi kwa wafanyabiashara wote KCB tunafungua fursa , tunafungua milango waje na mawazo ambayo wanaweza kupewa fedha" amesema Bwa. Abdul 

WAFANYABIASHARA WA SHINYANGA WANASEMAJE


Mwenyekiti wa wafanyabiashara Shinyanga, Dkt. Kulwa Meshack amesema katika kipindi cha COVID-19 na vita ya Ukraine pamoja na Urus biashara ya mafuta imekuwa na changamoto kubwa kwasababu mafuta mengi yaliyokuwa yanakuja kutoka nje ya nchi sasa yamekuwa hayafiki na kwasababu hiyo mafuta pekee ambayo ni kimbilio ni mafuta ambayo yanazalishwa hapa nchini ikiwemo mafuta hayo ya alizeti ambayo hayana madhara mwilini.

Post a Comment

Previous Post Next Post