Mkurugenzi Mtendaji wa NGASMAKE CO LTD Emmanuel Ngalya akizungumza na Waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa huduma ya LIPA KWA UHAKIKA katika hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya TTCL Posta Jijini Dar es Salaaam tarehe 9 Juni 2022.
Mkurugenzi wa T-PESA BI. Lulu Mkudde akizungumza na Waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa huduma ya LIPA KWA UHAKIKA katika hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya TTCL Posta Jijini Dar es Salaaam tarehe 9 Juni 2022.
Viongozi wa Kampuni ya NGASMAKE CO LTD na Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa huduma ya LIPA KWA UHAKIKA katika hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya TTCL Posta Jijini Dar es Salaaam tarehe 9 Juni 2022.
Kaimu Meneja wa Uhusiano Shirika la Mawasiliano Tanzania, TTCL Edwin Mashasi akiongoza kikao wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya LIPA KWA UHAKIKA katika hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya TTCL Posta Jijini Dar es Salaaam tarehe 7 Juni 2022.
PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI- SAUTI ZA MTAA BLOG
********************************************
NA YUSUPH DIGOSSI- SAUTI ZA MTAA BLOG
kufuatia changamoto za kiusalama katika biashara za kimtandao ( Online Business) kwa mnunuzi na muuzaji ikiwemo udanganyifu na utapeli katika biashara pamoja na mnunuzi kupata huduma au bidhaa isiyo na kiwango kampuni ya NGASMAKE Co. Ltd imekuja na suluhisho la kutatua changamoto hii baada ya kuzindua mfumo salama wa LIPA KWA UHAKIKA .
Mfumo huu umeripotiwa kuwa utamsaidia mnunuzi na muuzaji kuwa salama katika biashara za mtandao ( online Business) na kuondoa changamoto ya udanganyifu, utapeli na bidhaa zisizokuwa na kiwango.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika katika Ofisi za Shirika la Mawasiliano Tanzania Jijini Dar es salaam leo Alhamisi Juni 9, 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa NGASMAKE CO LTD , Emmanuel Ngalya amesema kuwa huduma hiyo ni ya kipekee hapa nchini ambayo inatoa usalama kwa wauzaji na wanunuzi wa bidhaa na huduma kimtandao.
" Kuwepo kwa changamoto za kiusalama katika biashara za kimtandao haswa utapeli na mnunuzi au kupata bidhaa isiyo na kiwango ndio sababu ya kampuni yetu kuja na suluhisho la mfumo huu rafiki ambao utamsaidia mnunuzi na muuzaji kuwa salama katika Biashara " Amesema Bw. Ngalya
MFUMO UNAFANYAJE KAZI?
Akizungumzia namna mfumo huo unavyofanya kazi Mkurugenzi huyo amesema kuwa mnunuzi baada ya kununua bidhaa na kulipia kupitia T-PESA , fedha hizo zitaenda moja kwa moja kwa muuzaji na zitahifadhiwa kwenye mfumo mpaka mnunuzi atakapopata bidhaa yake na Kuthibitisha kuwa ni bidhaa yenyewe aloagiza ndio mfumo utaruhusu fedha hizo kwenda kwa muuzaji.
FAIDA ZA MFUMO KWA MNUNUZI NA MUUZAJI
Ngalya amezitaja faida za matumizi ya mfumo huo kwa mnunuzi wa bidhaa mtandao ni pamoja na pesa ya mnunuzi kuwa salama hadi apate au huduma yake na ataweza kurudisha malipo yake ikiwa bidhaa haijawalishwa.
Kwa upande wa Muuzaju, Ngalya amesema uhakika wa malipo mara tu wanapowasilisha bidhaa au huduma pamoja na kupokea taarifa ya malipo kabla ya kutoa huduma.
WITO KWA WATANZANIA
Kampuni ya NGASMAKE CO LTD imetoa wito kwa watanzania kutumia huduma hii ya LIPA KWA UHAKIKA kwakuwa ni mfumo salama na rafiki kwa watumiaji kwasababu unalinda usalama wa fedha za mnunuzi.
USHIRIKI WA TTCL KATIKA UZINDUZI WA MFUMO HUU
Shirika la Mawasiliano Tanzania, TTCL kwa kushirikiana na kampuni ya NGASMAKE wamewezesha mfumo LIPA KWA UHAKIKA ambapo watakua wanafanya kazi kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa T-PESA BI. LULU MKUDDE amesema huduma hiyo itaondoa kilio cha muda mrefu cha wanunuzi wa bidhaa kutopata bidhaa zoa ikiwa tayari wamekwishafanya malipo.
Ameongeza kuwa kupitia kupitia mfumo huo utazisaidia kuzuia udanganyifu na utapeli.
WITO WA TTCL KWA WANUNUZI
TTCL imetoa rai kwa wanunuzi wa huduma au bidhaa kupitia mitandao ya kibiashara ambayo hupatikana hapa nchini kutumia mfumo wa LIPA KWA UHAKIKA ambao unahahakikisha usalama wa fedha zao.
Katika hatua nyingine Bi. Lulu aliyasihi makampuni au watu binafsi wenye mawazo ya kibunifu kwenye sekta ya mawasiliano kufika TTCL kwakuwa Shirika hilo lina mifumo salama na ya uhakika.
Tags:
BIASHARA