AMREF YAZINDUA MBIO ZA BAISKELI, KUCHANGISHA FEDHA KUSAIDIA HUDUMA ZA AFYA



Na Yusuph Digossi- Sauti za mtaa Blog 

Mbio za baiskeli zijulikanazo kwa jina la 'Africa Classic ' zinazoratibiwa na shirika la Amref Netherlands kwa kushirikiana na Amref Africa  zimefunguliwa rasmi leo Jumapili , Juni 12, 2022 Mkoani Kilimanjaro. 

Katika mbio hizo Raia zaidi ya 40 wameanza mbio hizo kwa kuzunguka mlima Kilimanjaro kilometa 400 kwa siku sita kuanzia juni 12 hadi 18 kwa awamu  ya kwanza na awamu ya pili itafanyika Juni 19 hadi 25 ambapo waendesha baiskeli 67 watashirika mbio hizo.

Mbio hizo zinalenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za Afya zilitambulishwa katika nyumba ya kulala wageni ya Kia iliyopo Mkoani Kilimanjaro na Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Jairy Khanga.


Akizungumza leo Jumapili Juni 12, 2022 katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Amref Health Africa, Anthony Chamungwana amesema mbio hizo za kuendesha baiskeli zilianza rasmi miaka saba iliyopita  ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia sekta ya Afya Tanzania na mafanikio makubwa yameonekana.


Ameongeza kuwa Amref Health Africa Uholanzi imekuwa ikisaidia miradi na matukio yenye athari kubwa ikiwa ni pamoja na tukio hili la kuendesha baiskeli barani Afrika ambalo hukusanya kiasi kinachoweza kudaiwa cha fedha kwa ajili ya suluhu za afya.

"Tunashukuru kwamba Amref Tanzania ni miongoni mwa wanufaika wa hazina hiyo   na tunataka kuwahakikishia kwamba, tunathamini jitihada zenu hasa mipango ya kukusanya fedha ambayo mnapigania kusaidia Waafrika kupitia afua mbalimbali za afya." amesema Chamungwana .


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkazi was Amref Tanzania Gaspar Jonah, amesema kuwa mchezo huo  umekuwa ukifanywa kila mwaka lakini kwa miaka 2 iliyopita haikuwezekana kutokana na mlipuko wa COVID-19, huku akiwapongeza , washiriki kwa kuwa na  subira  hadi  wakati huu tena na kujitokeza kushiriki mchezo huo. 

 
"Uongozi wa Amref  unathamini Mamlaka ya Kilimanjaro kwa kujitolea na uungwaji mkono unaotolewa kwetu kila wakati, hili halingewezekana bila    ushirikiano wako, tutaendelea kukuarifu na kutafuta mwongozo wako wakati wowote mpango/fursa za aina hii za kusaidia jumuiya yetu   zinapotokea". amesema Gaspar.


Naye  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Jairy Khanga amewashukuru waendesha baiskeli hao kwa kujitolea na ukarimu wao wa kusafiri hadi Tanzania ili kusaidia kuboresha afya za wananchi wa Tanzania.

“Napenda kuwahakikishia kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono mpango huu muhimu, kwa kufanya kazi kwa karibu na Amref Health Africa. Tunathamini na kutambua uhusiano mzuri wa kufanya kazi na ushirikiano kati ya Serikali na Amref Health Africa. amesema Dr Jairy Khanga.


Post a Comment

Previous Post Next Post