MAMBO YAZIDI KUNOGA KUELEKEA SERENGETI MUSIC FESTIVAL WASANII ZAIDI YA 200 WAKUTANISHWA KWENYE ROYAL DINNER



Na John Mapepele


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamishna wa Sensa  nchini Mhe. Anna Samamba Makinda amekuwa miongoni mwa  wageni walioshiriki usiku wa  chakula  cha pamoja uliowakutanisha  wasanii zaidi ya 200 wanaotarajia kutumbuiza kwenye Tamasha kubwa dunia la Muziki la Serengeti linalofanyika jijini Dodoma Machi 12 na 13, 2022.


Dhifa hiyo ya chakula cha jioni imekuwa ya aina yake ambapo wasanii wamepata fursa ya kuelimisha  umuhimu wa sensa.

Aidha, kuelekea kesho  kwenye  tamasha la Serengeti  wasanii mbalimbali wakiongozwa na Bushoke wamekonga nyoyo za  wa wageni mbalimbali walioshiriki usiku huu.



Mbali na  viongozi Wakuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo,wageni wengine ni wabunge na wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha na binafsi na watu mashughuli.


Aidha, wasanii wamepata nafasi ya kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa makampuni walioshiriki.

Mdhamini Mkuu wa shughuli hii ni CRDB.

Serengeti inakwenda kufanyika kesho ikiwa ni mwaka mmoja toka kuingia madarakani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.




Post a Comment

Previous Post Next Post