Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), DKt. Stephan Ngailo akizungumza na kikundi cha wakulima cha Jitegemee katika Kata ya Mnacho alipofika kukagua maendeleo ya mashamba ya mfano na ya wakulima hao katika kuhamasisha matumizi ya mbolea katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi tar 10 March, 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), DKt. Stephan Ngailo wa pili kulia akizungumza na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Lindi, Majid Myao alipofika ofisini kwake kuzungumzia maandalizi ya siku ya mkulima katika mkoa huo.Wanakikundi wa jitegemee wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), DKt. Stephan Ngailo (hayupo pichani) aliyefika kukagua maendeleo ya mashamba katika eneo la Mnacho wilayani Ruangwa.
Mmoja wa mwanakikundi cha Jikomboe akiwa katika shamba la mfano katika eneo la Mbemba Chigugu wilayani Masasi. Nyuma ni mahindi yaliyopandwa kwa kutumia mbolea na mbele hayajatumia mbolea.
Swalehe Tendwa (katikati) Bwana shaamba kata ya Kitere akieleza jambo kuhusu kilimo cha mpunga kwa viongozi walioambatana na Mkurugenzi wa TFRA Dkt. Stephan Ngailo(hayupo pichani) alipofanya ziara katika mashamba hayo kuona manufaa ya matumizi bora ya mbolea katika kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), DKt. Stephan Ngailo (kushoto) akimsikiliza Swalehe Tendwa ( wa pili kulia) Bwana shamba kata ya Kitere alipofika kukagua maendeleo ya mashamba hayo tarehe 11 March, 2022.