TCD yazindua Jukwaa la majadiliano ya vyama vya siasa ngazi ya Wilaya

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (kushoto) akisalimiana na Msaidizi wa Masuala ya Siasa na Uchumi kutoka Ubalozi wa Marekani Bw. Bion Bliss (kulia) wakati wa uzinduzi wa majukwaa ya majadiliano ya vyama vya siasa Wilaya ya Ilala kuhusu demokrasia ya vyama vingi leo Jumatatu Febuari 6, 2023 katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.


Msaidizi wa Masuala ya Siasa na Uchumi kutoka Ubalozi wa Marekani nchini (Deputy Political and Economic Affairs chief at the US Embassy) akizungumza wakati wa uzinduzi wa majukwaa ya majadiliano ya vyama vya siasa Wilaya ya Ilala kuhusu demokrasia ya vyama vingi leo Jumatatu Febuari 6, 2023 katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Bi. Bernadetha Kafuko akizungumza wakati wa uzinduzi wa majukwaa ya majadiliano ya vyama vya siasa Wilaya ya Ilala kuhusu demokrasia ya vyama vingi leo Jumatatu Febuari 6, 2023 Karimjee Jijini Dar es salaam.

Na Yusuph Digossi - Sauti za Mtaa Blog

Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Mwanachama wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 06, 2023 mara baada ya kuzindua Jukwaa la Majadiliano ya vyama vya siasa Wilaya ya Ilala.

Makamu mwenyekiti wa  Kituo cha Demokrasia Tanzania TCD Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa mfumo wa Demokrasia imara ni ule unapfanya maamuzi ya kugusa maisha ya watu kuanzia ngazi ya chini huku akisistiza kuwa maamuzi hayo ni muhimu sana katika kuimarissha ustawi wa demokrasia nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Mwanachama wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 06, 2023 mara baada ya kuzindua Jukwaa la Majadiliano ya vyama vya siasa Wilaya ya Ilala.


Prof. Lipumba ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa majukwaa ya majadiliano ya vyama vya siasa Wilaya kuhusu demokrasia ya vyama vingi  leo Jumatatu Febuari 6, 2023 Jijini Dar es salaam.

Lipumba amesema nchi yenye mfumo imara wa Demokrasi inafanya maamuzi yanayowahusu wananchi karibu na wananchi wenyewe na kusisitiza mwaka 2024 wadau wa siasa wanatarajia uchaguzi ulio huru na haki na unaozingatia misingi ya katiba.

Aidha Lipumba amehimiza umoja na mshikamano kwa viongozi vyama vya siasa ili nchi ya Tanzania iwe mfano katika mfumo wa demokrasia na uchaguzi unaozingatia katiba na kuwaletea wananchi maendeleo

Kwa upande wake Zitto Kabwe alisema rais Samia alitoa wito wa maridhiano, mageuzi, ustahimilivu na ujenzi mpya wa Taifa ambapo alisema kupitia majadiliano hayo yatasaidia kujenga Taifa la watu ambao wamezungumza, wanasikilizana, wanaweza kutatua matatizo yai mezani na siyo barabarani na hivyo kujenga Taifa imara na la kidemokrasia.

"Naamini kwamba chini ya Uongozi wa TCD chini ya Mwenyekiti wake, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti, Prof. Lipumba nchi hii itakaa kwenye meza ya majadiliano ya pamoja, tuwaombee kuelekea kwenye maridhiano na majadiliano." amesema Zitto.





Post a Comment

Previous Post Next Post