NEMC YAENDELEA NA UTAFITI KUDHIBITI TAKA NGUMU NCHINI



Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesema kuwa linaendelea kufanya utafiti juu ya udhibiti wa taka ngumu kwasababu limekua tatizo sugu ambalo linachangiwa na kuongezeka kwa madampo.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Januari 23, 2023 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka wakati wa zoezi la kusaini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Taasisi inayojishughulisha na masuala ya kisayansi na kimazingira kutoka nchini India ambapo ushirikiano huo utasaidia kufanya maboresho katika ukusanyaji wa taka ngumu.


Gwamaka amesema nia ya mkataba huo uwe wa miaka mitatu kuanzia sasa lakini kutakuwa na uwezekano kuupeleka mbele zaidi lengo kubwa ni kuzipa nguvu Mamlaka za Serikali za Mitaa hasa katika majiji, miji pamoja na Wilaya ndo maana wakurugenzi wameweza kushiriki kwenye mkutano huo ili waweze kubadilishana mawazo na uzoefu ili baadae tuwe na mifumo ya kisasa kuhakikisha taka ngumu zinazozalishwa ziwezwe kutengwa na zisionekane kwenye madampona zile zinazooza ziweze kuwa mbolea

"Moja ya jitihada zinazofanywa na taasi yetu ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa taka ngumu kwa lengo la kuzibadili ziweze kutumika katika nyanja ya maendeleo" Amesema Gwamaka


Kwa upande Wake Muwakilishi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bi. Hawa Mwechaga amezitaka Halmashauri zote nchini kuwa na mpango mkakati wa kutokomeza taka ngumu katika maeneo yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post