Diwani Job Isack wa kata ya Mzinga iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Ilala amesema Ujenzi wa Kituo hicho unaendelea vizuri na matarajio ni katika kipindi hiki cha mwaka 2020-2025 kitakuwa kimekamilika.
Akizungumzia leo juu hatua hizo za ujenzi amesema utekelezaji hupokatika tathimini nzuri ambpo mkandarasi aliyepewa dhabuni hiyo yupo site akitekekeza majumuku yake .
“Lengo la serikali ni kuona huduma za afya zikitolewa kwa uhakiki zaidi katika kuwa huduma bora wananchi wake hivyo nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kuchohea maendeleo ili kutimiza ilani ya chama cha mapinduzi,”amesema Mhe.Job.
Jobu amesema hadi sasa takribanai miradi mingi ya ujenzi imefanyika katika kata yake hivyo kufanya huduma za jamii kupatikana kihurahisi .
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga, Nyaikoba Ryoba wa kata hiyo ya Mzinga amesema kata hiyo inapakana na kata ya Kitunda upande wa Kaskazini, Kusini inapakana na Chamazi iliyopo manispaa ya Temeke. Upande wa mashariki inapakana na Buza huku kaya ya Mzinga ikiwa na Jumla ya wananchi elfu 42 .
“Natumaini kuwa kukamilika kwa ujenzi kutaweza kufanya huduma za afya kuwa bora zaidi ambapo huduma hiyo itavuka mipaka kwa baadhi ya wananchi wa maeneo jirani niliyoyataja kuweza kupata huduma ya afya katika kituo hicho cha afya mara tu , kitakapo kamilika ,”amesema Ryoba.
Wakati huo huo mmoja wa mhandisi mwajiliwa wa Halmashauri ya hiyo ya Jiji la Ilala , Hatari Marosa amesema kuwa hadi sasa hatua za ujenzi zinaendelea vizuri kwa kuwa mradi huo umefikia asilimia 80 .
“Makandarasi amefikia asilimia 80 katika floo ya kwanza aliyopewa ambapo ametumia jumala ya Mil 200 hadi sasa na endapo halmashauri inaweza kuendelea naye itampatia tena kuendelea na hatua nzingine za ujenzi wa floo ya 2,”amesema Mhandisi Marosa.
Naye mwandisi anaye mwenye dhabuni na mradi huo wa huduma ya afya Edyson Stanley amesema hadi sasa anashukuru kwa hatua za ujenzihuo kuendelea vizuri.
Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Mwenyekiti wa tawi la Magole B Victor Lyamuya amempongeza Mhe.Job kwa juhudi za kuhamasisha maendeleo katika kata hiyo .
“Katika uongozi wake akishirikiana na viongozi wengine wa chama na serikali Job amepambania ujenzi wa shule mpya ya Sekondari na ikiwezekana huku shule ya Msingi akiipanua zaidi kwa kuongeza majengo mapya tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.”
Tags:
HABARI