Kufuatia ziara aliyoifanya na Rais samia nchini Misri imeonekana kuzaa matunda baada ya wawekezaji kutoka nchini humo kuonyesha nia ya kuwekeza nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu Afisa Mtendaji wa kampuni ya GS Group na mmoja wa wawekezaji Gassey El-Sayed, ameonesha nia ya kuwekeza katika eneo la VEHICLE INSPECTION CENTERS na TRAFFIC Management Solutions Kwenye Mikoa Yote Tanzania Kwa Njia ya PPP.
Mkuu huyo wa kampuni hiyo, El-Sayed alisema kwa sasa wameanza kufuatilia vibali, Utaratibu na kanuni zote za uwekezaji Kutoka Serikalini kabla ya kuanza Uwekezaji huo nchini.
"Baada ya Ziara Ya COP27 Ya Mh Rais Wa Tanzania Egypt, Tumeona ni Fursa Njema Kuleta Uwekezaji Wetu Tanzania Kama Tulivyofanya Ghana, Chad, Nigeria, Dubai na Saudi Arabia, na tumekusudia kuja Kuwekeza katika kwenye eneo la VEHICLE INSPECTION CENTERS na tutajikita zaidi katika masuala ya usalama barabarani ambapo tutatumia mageuzi ya kidigitali katika kufanya shughuli hiyo" ambapo Mbali na kusaidia Mazingira Mradi Huu Utaisaidia Serikali Kukusanya Mapato Kwa Ajili ya Maendeleo ya Nchi Kama Ilivyokuwa Kwenye Nchi Nyingine ambapo Mapato Yaliongezeka Kwa Asilimia 60% Baada ya Uwekezaji wao alisema El-Sayed.
El-Sayed alisema katika kutekeleza suala hilo watajenga mitambo maalumu Nchi Nzima ambazo zitatumika kukagua magari yote na vyombo vingine vya moto kama pikipiki ambavyo vitakuwa havina ubora, kama kutoa moshi na uchakavu na kuhakikisha Usalama wa barabarani.
Alisema kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Afrika na imekuwa ikijishughulisha kutengeneza mbolea, masuala ya afya, bidhaa za ngozi, na kwa sasa wana mkataba wa kutengeza Pia Vifaa Vyote vinavyotumika Kwenye World Cup Qatar na FIFA ikiwemo mipira na mambo mengine mbalimbali.
Aliongeza kuwa tayari kampuni hiyo imekuwa ikifanya majadiliano na Serikali kwa takribani Mwaka na Nusu sasa na wana Imani michakato Iko Kwenye Hatua za Mwisho kuhusu maswala na maeneo ambayo serikali itawapendeza kufanya Uwekezaji huo na kwa awamu ya kwanza wataanza na kazi hiyo na baadae iwapo watakubaliwa wataingia katika masuala mengine ikiwemo Kujenga Viwanda na Kujenga Mifumo MbaliMbali Ya Kuweza Kusaidia Serikali Kwenye Ukusanyaji Wa Mapato.