SHERIA YA HUDUMA ZA VYOMBO VYA HABARI HAIJAKIDHI VIWANGO VYA HAKI ZA BINADAMU




Na Yusuph Digossi

Afisa Uchechemuzi kutoka kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu (LHRC ), Raymond Kanegene amesema nia  ya serikali kubadilisha sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 inatia moyo  kutokana na kikao cha Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nnauye na wadau wa vyombo vya habari  kilichofanyika siku za hizi karibuni.

Kanegene ameyasema hayo Leo Alhamisi Novemba 24 Jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu aliyofanya na Sauti za Mtaa Blog kuhusu mchakato wa  mabadiliko ya sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 .

Afisa Uchechemuzi huyo ameeleza kuwa  shauku ya wadau wengi wa vyombo vya habari ni kuona sheria hiyo inabadilishwa kwasababu ni sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari na haikufikia viwango vya haki za binadamu.

Amesema " mwaka 2018 kulikua na maamuzi ya kesi iliyofunguliwa kuhusu sheria ya vyombo vya habari na mahakama ya Africa mashariki ilisema kuwa sheria hiyo haifikii viwango vya haki za binadamu kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa haki za binadamu Afrika Mashariki" 

Ameiambia sauti za mtaa  kwa kiwango fulani Serikali imekubali maoni ya wadau kuwa ni sahihi na imeanza mchakato wa kubadilisha baadhi ya vifungu kandamizi vya sheria hii.


"kifungu kilichompa mamalaka  Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo kufuta au kusimamisha huduma za vyombo vya habari ni vifungu vilivyokua kandamizi kwa muda mrefu hivyo vinatakiwa kufutwa" amesema 

Amebainisha kufutwa kwa vifungu hivyo kutaleta hali ya kufikia viwango vya haki za binadamu kwasababu vyombo vya habari ni nyenzo muhimu ya kuweza kuibua masuala mbalimbali katika jamii hivyo vinatakiwa kuwa huru ili kuleta maendeleo.

Post a Comment

Previous Post Next Post