TRA YALENGA KUKUSANYA TRILIONI 23.65 KWA MWAKA WA FEDHA 2022- 2023



Timothy Marko

Katika Mwaka wa Fedha wa 2022/2023  Mamlaka ya Mapato  nchini (TRA) imelenga kukusanya Shilingi trioni 23.65 ambayo ni sehemu ya Serikali ya shilingi trioni 41.4 ikilinganishwa  na shilingi trioni 22.99 katika Makusanyo  ya Mwaka 2021/22.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema Makusanyo hayo Asilimia 99.22 ya Malengo yametokana Maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan inayowataka taasisi hiyo kukusanya Kodi kwa Weledi  na kukaa na walipakodi kwa kutatua changamoto zao ikiwa kuweka Mazingira Rafiki ya kulipa kodizao pamoja   kuongeza Kasi ya kupanua wigo kwa kuwasajili walipakodi wapya.


"Mwaka Jana tulizidi kuwekeza kwenye Tehama na uanzishwaji wa Mfumo wa kuwasilisha ritani za VAT kieletroniki ambao umeongeza ufanisi nakuondoa Mapungufu na udanganyifu".

 Alisema Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Kodi Richard Kayombo.

Kayombo Alisema kuwa katika Mwaka huu wa Fedha wa 2022/23 taasisi hiyo imelenga kutoa Elimu kwa Watumishi na wafanyabishara nchini juu ya Mabadiliko Mbalimbali ya sheria za Kodi sambamba natozo pamoja na Ada zinazo simamiwa na taasisi hiyo katika kuratibu taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa Mapato ya Serikali.


"Marekebisho haya ya sheria za Kodi yamelenga kusaidia kuongeza Kasi ya kufufua Uchumi na kuimarisha Sekta za Uzalishaji kwa ajili ya kuboresha Maisha."Aliongeza Richard Kayombo.

Kayombo Alisisitiza kuwa katika Mwaka huu wa Fedha TRA imelenga kufanyia Marekebisho ya Sheria ya ushuru wa Bidhaa sura 147, Sheria ya Magari ya kigeni sura 84 Sheria ya Kodi Mapato sura 332 ,Sheria ya Ongezeko la Thamani Sura 148.

Alibainisha kuwa Sheria zingine Sheria ya usimamiziwakodi sura 438 ,sheria ya Madini sura 123 , Sheria usafirishaji Bidhaa nje ya nchi sura 196 , Sheria ya Posta na Mawasiliano ya kieletroniki sura 306, Sheria usimamiziwa Forodha ya Jumuhia ya  Afrika Mashariki ya 2004 na Sheria nyingineza Mapato ya siyo ya Kodi.

Post a Comment

Previous Post Next Post