MGUMBA AIPONGEZA KAMPUNI YA GBP KWA UWEKEZAJI MKUBWA



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameipongeza kampuni ya mafuta ya GBP kwa uwekezaji mkubwa inayoendelea kuufanya  ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa na mchango mkubwa kwa Maendeleo ya mkoa na kuchangia pato la  taifa.

Mgumba alitoa pongezi hizo ikiwa ni mara ya kwanza ya ziara zake kutembelea na kujionea miradi mbalimbali Mkoani Tanga ambapo alisema kuwa adhima ya serikali ni kufungua uchumi pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji  ambao wamekuwa ni wadau wakubwa wa maendeleo.

Mgumba alisema kuwa Tanga ambayo Sasa imekuwa ni kivutio kikubwa kwa wawekezaji kutokana na ujio wa Bomba la mafuta  wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaendelea kuweka mazingira rafiki pamoja na kuondoka vikwazo kwa wafanyabiashara wa mafuta hapa nchini kuitumia bandari ya Tanga.
 


"Niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na sisi serikali inafarijika na uwepo wenu mna mchango mkubwa kwenye taifa hili kiuchumi pamoja na kutoa ajira kwa watanzania na mimi kwakuona hilo ninawatakia kila la kheri" alisema Mgumba.

Mara baada ya Mkuu wa Mkoa  kutembelea bohari ya mafuta ya GBP uongozi wa bohari hiyo umemuomba kuingilia kati viwango vya bei vya EWURA  ambavyo vinasababisha wafanyabiashara wa mafuta kanda ya kaskazini  kuchukulia bidhaa hiyo  bandari ya Dar es Salaam  badala ya bandari ya Tanga. 


Akizungumza  meneja wa kampuni hiyo  Fahimu Salimu alisema kuwa wanaendelea kuboresha miundombinu  katika bohari yao ili kuwawezesha kutoa huduma kwa wafanyabiashara wa mafuta hapa nchini huku wakiwa wanatoa magari 80  ya mafuta kwa siku.


Aidha amezitaja baadhi ya  changamoto zinazowakabili ambapo alisema kuwa kuchelewa kwa meli ya mafuta kuja hapa nchini inapelekea kushindwa kutoa huduma hiyo kwa ufanisi.

"GBP  ni moja ya kituo kikubwa cha mafuta na uwezo wake ni mkubwa tulibadilisha miundombinu yetu ya mabomba Mara nyingi  meli ukichelewa inakuwa ni changamoto na hasara kwetu sisi" alisema


Post a Comment

Previous Post Next Post