DKT.MAGEMBE AWAJIA JUU KILWA NI KUHUSU KUSUA SUA KWA MIRADI YA AFYA




OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Dkt.  Grace  Magembe amesema  hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma  za afya unaotekelezwa katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Amesema kuwa Ofisi ya Rais- TAMISEMI itafanya uchunguzi wa kina  katika miradi  ambayo imeonekana  kuwa na  mapungufu  na  yoyote atakayebainika kurudisha nyuma  utekelezaji huo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi wa umma.

Hayo yamebainishwa tarehe 24 Julai 2022 katika ziara yake  ya  kukagua ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya  katika Hospitali ya Wilaya ya Kinyonga, Kituo cha afya Hoteli tatu pamoja na Kituo cha Afya  Kipindimbi zilizopo katika Halmashauri ya Kilwa.


 “ Lengo la Serikali ni kuhakikisha  wananchi wanapata huduma bora za afya,  kutokamilisha miradi  kwa wakati ni kwenda kinyume na azma ya  Serikali ya awamu ya sita ya kumsogezea  mwananchi huduma bora ” Dkt.Magembe

 Aidha pamoja na ucheleshwaji huo ,  Dkt. Magembe  ameitaka Halmashauri ya Kilwa kuzingatia maelekezo  na maagizo yanayotolewa na Serikali  katika utekelezaji wa miradi  hasa katika matumizi ya fedha ili fedha hizo zitumike kama ilivyopangwa na Serikali .

“ Ukiangalia   Kituo cha Afya Kipindimbi Mil. 250 zilitakiwa zijenge  jengo la wagonjwa wa nje, maabara pamoja na kichomea taka  lakini kichomea taka hakijajengwa na fedha zimeisha. Hapa Hoteli tatu  kichomea taka hakijajengwa, uchunguzi utakaofanyika utatuambia kwa nini mmeshindwa kutekeleza miradi hii kama Serikali ilivyoelekeza “ Dkt. Magembe


Pamoja na hayo Dkt. Magembe amewapongeza wananchi wa maeneo ya miradi kwa kuunga  mkono juhudi za Serikali  katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa  kuimarisha  ulinzi na  usimamizi wa miradi   pamoja na kuchangia nguvu kazi katika utekelezaji.


Post a Comment

Previous Post Next Post