TFRA yakiri upatikanaji mzuri wa mbolea Nyanda za Juu Kusini




Kaimu Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini- Mbeya Michael Sanga akiambatana na watumishi wa ofisi yake leo tarehe 16 Mei, 2022 wametembelea maghala ya kampuni ya mbolea ya ETG na kubaini uwepo wa mbolea ya kutosha katika maghala hayo. 

Uongozi huo umefanya ziara hiyo ikiwa ni ukaguzi wa kawaida wenye lengo la kujionea endapo biashara ya mbolea inafanyika kwa kufuata sheria na taratibu zinazosimamia tasnia hiyo.

Akitoa takwimu za mbolea iliyopo katika maghala ya ETG Sanga alisema kuna mbolea aina ya DAP tani 208.78, UREA tani 99.68, N:P:K tani 313.10, TSP tani 58.25, SA tani 25.55, MOP tani 20.8 na KYNOPLUS tani 0.85.


Post a Comment

Previous Post Next Post