BASHUNGWA AKERWA NA KASI NDOGO YA UJENZI JENGO LA UTAWALA MOSHI DC




Angela Msimbira - KILIMANJARO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Innocent Bashungwa aagiza kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya wilaya ya Moshi  ifikapo tahe 24 Juni, 2022 kulingana na mkataba uliopo.

Ametoa agizo hilo jana wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro

Bashungwa amemuagiza Mkandarasi SUMA JKT kuongeza nguvu kazi na  kasi ya ujenzi ili jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati kulingana na mkataba wa ujenzi huo.


"Mheshiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo lakini watendaji wamekuwa wakichelewesha miradi hiyo na kurudisha nyuma maendeleo ya  wananchi,  niwaagize viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia ujenzi huo na kuhakikisha linakamilika kwa wakati" amesisitiza Waziri Bashungwa

Aidha,  mradi wa ujenzi wa jengo la utawala umekadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.9



Post a Comment

Previous Post Next Post