SHOMBE: NDC NI MKONO WA SERIKALI KWENYE UWEKEZAJI NA INA NAFASI KUBWA YA KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa NDC Dkt. Nicolaus Shombe akizungumza na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bi Miriam Chavalla mara baada ya kutembelea banda hilo  katika Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa NDC Dkt. Nicolaus Shombe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda hilo  katika Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Maendeleo NDC Bi Miriam Chavalla  akimueleza jambo Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Dkt. Nicolaus Shombe  mara baada ya kutembelea banda la NDC  katika Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.



Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC Bi. Miriam Chavalla akimpa akimpa maelezo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo Dkt. Nicolaus Shombe kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na NDC mara baada ya kutembelea banda lao katika maonesho ya pili ya bidhaa za wajasiriamali wanawake yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. ( Picha zote na Iddy Lugendo) 




Na Yusuph Digossi- Sauti za Mtaa Blog 

Dar es Salaam 

Imeelezwa kuwa Shirika la Taifa la Maendeleo  NDC ni mkono wa serikali kwenye uwekezaji kwa kushirikiana na sekta binafis na lina nafasi kubwa ya kuchangia katika maendeleo ya sekta  viwanda nchini Tanzania. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la  Maendeleo ( NDC ), Dkt. Nicolaus  Shombe alipotembelea banda la shirika hilo  kwenye maonesho ya bidhaa za wajasiriamali wanawake yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa NDC inawekeza katika viwanda vya msingi ambavyo vinaleta matokeo chanya kwenye viwanda vingine kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na NDC ikwemo mradi wa makaa ya mawe, mpira na magadi soda imekuwa na  mchango mkubwa katika maendeleo ya Sekta ya Viwanda Nchini. 

" NDC tumekuwa tukiwekeza katika maeneo ya kimkakati kwa kushirikiana na sekta binafsi kwenye Viwanda ambavyo vinaleta tija katika viwanda vingine , mfano mradi wa magadi soda ndio kila kitu katika sekta ya viwanda hapa nchini " amesema Shombe 

Ameongeza kuwa NDC inafanya biashara ya kupeleka bidhaa nje ya nchi kama vile Angola, Nigeria, Kenya,  Swaziland na maeneo mengine. 

Ameeleza kuwa lengo ni kuwa na NDC mpya ambayo italeta tija kwenye maendeleo ya uchumi wa nchi kutokana na miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo.  

Akizungumzia uwepo wa banda la NDC katika maonesho ya bidhaa za wajasiriamali mali wanawake yanayoendelea katika Viwanja amesema vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam Shombe amesema kuwa lengo  kuendelea kuwashika mkono Wanawake ambao wana mchango mkubwa katika shughuli za maendeleo ya Taifa.


Post a Comment

Previous Post Next Post